Kocha mpya Chelsea achimbwa mkwara mzito

Friday July 20 2018

 

LONDON, ENGLAND. KOCHA, Maurizio Sarri ameambiwa hivi na bosi wake mpya huko klabuni Chelsea, Roman Abramovich kwamba anapaswa kubadili tabia baada ya kuchaguliwa kuchukua mikoba ya Antonio Conte huko Stamford Bridge.
Sarri ameambiwa hivi, kwanza anapaswa kuvaa suti katika kila mechi na kuachana na ile desturi ya kuvaa tracksuit na pia afute kabisa ile kawaida yake ya kwenda kuvuta sigara wakati wapumziko.

Kocha Sarri alikuwa akipuliza tu sigara kwenye mechi alipokuwa Napoli kabla ya kupigwa marufuku kufanya hivyo. Bilionea Abramovich sasa anamtaka kuacha kuvuta sigara wakati wa mapumziko na avae suti kwenye mechi.

Advertisement