Kisa mchepuko! Kiprop amuomba radhi mke wake

Thursday September 20 2018

 

By THOMAS MATIKO

BINGWA mara tatu wa dunia kwenye mbio za mita 1,500, Asbel Kiprop amempigia magoti mke wake na kumwomba msamaha akimtaka arejee nyumbani kufuatia skendo yake ya mchepuko.

Majumaa kadhaa yaliyopita kuliibuka video mtandaoni inayoonekana Asbel akinyonyana ndimi na mwanamke mmoja aliyefungua shati lake akianika wazi sidiria kwa yeyote mwenye macho kutizama.

Wawili hao walionekana wakiwa ndani ya gari na Asbel ndiye akirekodi video ile.

Baada ya kuvuja kwa video hiyo, Asbel alijitokeza na kukiri kumchepukia mke wake na mwanamke huyo kwa kipindi cha miaka miwili. Na mara tu ya kukiri, mke wake wa ndoa alifungasha na kuondoka.

Mpaka wa leo ikiwa imepita takriban miezi miwili mke wa Asbel hajarejea nyumbani na sasa mwanaridha huyo amempigia magoti akimwomba amsamaha.

“Nilikosea na kwa kweli namtaka mke wangu arejee nyumbani. Sijui ni nani aliyevuijisha video ile lakini pamoja na yote ninachotaka kwa sasa ni mke wangu arudi nyumbani. Kila nikimfuata ananikimbia. Ana hasira na mimi sana. Na kwa kuwa nimekuwa muwazi na kukiri kumchepukia kwa miaka miwili jambo ambalo hakuwahi kulifahamu, namwomba tu anisamehe na arudi nyumbani,” alisema Asbel.

Advertisement