Kipa Liverpool aunda kikosi ghali zaidi duniani

Friday July 20 2018

 

London, England. Kipa wa mpya wa Liverpool, Alisson ameingia katika kikosi cha wachezaji ghali zaidi dunia pamoja na Neymar, Cristiano Ronaldo na Kylian Mbappe.
Mbrazili Alisson ameivunja rekodi iliyokuwa ikishikiriwa kipa Ederson wa Manchester City baada ya uhamisho wake gharimu pauni 65milion kutoka Roma kwenda Liverpool.
Kikosi cha wachezaji hao 11 ghali wenye thamani ya pauni 992.65milioni sita kati yao wanatoka katika klabu zinazoshiriki Ligi Kuu England.

Kikosi cha wachezaji ghali kinaundwa:
Alisson (Roma kwenda Liverpool kwa pauni 65m)
Benjamin Mendy (AS Monaco kwenda Man City, pauni 51.75m)
Virgil van Dijk (Southampton kwenda Liverpool, pauni 70.1m)
Aymeric Laporte (Atletic Bilbao kwenda Man City, pauni 58.5m)
Kyle Walker (Tottenham kwenda Man City, pauni 47.5m)
Paul Pogba (Juventus kwenda Man United, pauni 94m)
Philippe Coutinho (Liverpool kwenda Barcelona, pauni 112.5m)
James Rodriguez (AS Monaco kwenda Real Madrid, pauni 67.5m)
Neymar (Barcelona kwenda PSG, pauni 199.8m)
Cristiano Ronaldo (Real Madrid kwenda Juventus, pauni 105m)
Kylian Mbappe (AS Monaco kwenda PSG, pauni 121m)

Advertisement