KMC kutesti mitambo na Wakenya

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, KMC keshokutwa Jumanne itatesti mitambo dhidi ya Kariobang Sharks ya Kenya ikiwa ni maandalizi ya mwisho mwisho kabla ya kuwafuata AS Kigali ya Rwanda.
KMC itaanza kibarua chake ugenini Agosti 10 itakapiovaana na wenyeji wao kwenye Uwanja wa Kigali na mechi yao na Wakenya itapigwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Meneja wa KMC, Water Harrison alisema wanaamini Sharks waliotoka sare ya bao 1-1 na Yanga jana kwenye Kilele cha Wiki ya Mwananchi ili kuwaandaa vijana wao kabla ya kuwafuata Wanyarwanda watakaovaana nao wikiendi hii.
"Tunaendelea na maandalizi na timu ipo vizuri hatuna majeruhi hata mmoja na tayari tumeshatangaza kikosi cha wachezaji 28 watakaoitumikia timu yetu kwa msimu wa mwaka 2019/20," alisema.
Walter alitaja kikosio hicho kuwa ni Ismail Gambo, Salim Aiyee, Serge Nogues, Basela Bukungu, Cliff Buyoya, Denis Richard, Abdul Hilary, Charles Ilanfia, Vitalisy Mayanga, Ally Ramadhan, Amos Kadikilo, Ally Msengi, Juma Kaseja, Kevin Kijili.
Wengine ni Rayman Mgungila, Boniphace Maganga, Rayman Mgungila, Jonathan Nahimana, James Msuva, Sadala Lipangile, Kenny Ally, Yusuff Ndikumana, Abdallah Mfuko, Ramadhan Kapera, Hassan Kabunda, Mohamed Samata, George Sangija, Melly Sivirwa na Jean-Baptise Mugiraneza.