Advertisement

Hata Rudiger naye kanogewa na Sarri

BEKI wa kati wa Chelsea, Antonia Rudiger amekiri wachezaji wote wa kikosi hicho cha Stamford Bridge wamepagawa na soka la kupiga mpira mwingi linalofundishwa na Kocha Maurizio Sarri klabu hapo kwa sasa.

IN SUMMARY

Sarri ameiongoza Chelsea kushinda mechi zote za kwanza walizocheza kwenye Ligi Kuu England, huku Rudiger akipangwa kwenye mechi hizo sambamba na David Luiz wakitengeneza ukuta mgumu kabisa katika kikosi hicho.

Wachezaji wa Chelsea wamempachika jina kocha wao wakimwita ‘Sarri-Ball’ kutokana na maagizo yake ya kuwataka wachezaji wake muda wote wawe na mpira na kupigia pasi nyingi na za uhakika.

“Niliichezea Roma huko Italia, hivyo nafahamu namna kocha anavyotaka kucheza soka lake, jambo ambalo binafsi linanivutia pia. Anataka tushambulie zaidi kuliko ilivyokuwa msimu uliopita ambapo timu ilikuwa inakaa nyuma tu kukaba,” alisema Rudiger.

“Kwa sasa mambo ni tofauti. Tumetengeneza nafasi nyingi na hilo ni jambo zuri. Zaidi kocha anahitaji mabeki wanaoucheza mpira, kupiga pasi fupi na kumiliki.”

More From Mwanaspoti
Advertisement
This page might use cookies if your analytics vendor requires them. Accept