Guardiola awakatisha tamaa mashabiki Man City

Muktasari:

  • Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, ambaye kwa mara ya kwanza aliiwezesha timu hiyo kufika 16 bora na baadaye kufikisha robo fainali katika misimu yake miwili ya kuinoa, amewaambia mashabiaki wa timu hiyo wasitarajie ubingwa wa Ulaya kwa sasa.

Manchester, England. Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amesema timu hiyo bado haina uwezo wa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Guardiola ambaye vijana wake leo wanaikaribisha Shakhtar Donetsk, alisema licha ya kiu kubwa waliyonayo mashabiki wa timu hiyo wanapaswa kuvuta subira ili kufikia mchakato wa kutwaa ubingwa huo.
Aliyasema hayo wakati akielezea maandalizi ya mechi yake ya leo itakayopigwa ugenini dhidi ya Shakhtar Donetsk ya Ukraine.
Man City inashika nafasi ya pili katika msimamo wa kundi F, ikiwa na pointi tatu moja nyuma ya vinara Lyon ya Ufaransa ambayo leo itachuana na Hoffenheim ya Ujerumani.
Akifafanua Guardiola alisema ili kutwaa taji hilo panahitajia nguvu na msukumo kutoka kwa kila mmoja kuanzia wachezaji, kocha, viongozi na mashabiki pia jambo ambalo kwa sasa halipo ndani ya City.
Kocha huyo alitwaa mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiinoa Barcelona ya Hispania lakini hakufanya hivyo alipoiona Bayern Munich.
Mechi zote za Ligi ya Mabingwa Ulaya zitakazopigwa leo ni AEK Athens vs Bayern Munich, Young Boys vs Valencia, Ajax vs Benfica, Hoffenheim vs Lyon, Manchester United vs Juventus, Real Madrid vs FC Viktoria Plzen, AS Roma vs CSKA Moscow na Shakhtar Donetsk vs Manchester City.