Eti hii ya Zidane ni sinema au?

Tuesday October 9 2018

 

STAA wa zamani wa Ufaransa, Bixente Lizarazu amesema stori za Zinedine Zidane kwenda kuinoa Manchester United ni sinema iliyotengenezwa vizuri na waandishi wa habari kuwavutia mashabiki wa timu hiyo.

Lizarazu amesema hakuna kitu kama hicho na uvumi huo uliozagaa kwamba Zidane atakwenda kurithi kiti cha Jose Mourinho huko Old Trafford ni kitu cha kufikirika, ni sinema tu za kwenye mpira wa miguu.

“Zidane kwenda Manchester United huu ni utunzi maridhawa wa waandishi, wanaishi na hisia na ndoto za mashabiki.

Imepigwa vyema ni sinema hii ya kwenye soka, hakuna ukweli hata kidogo,” alisema Lizarazu.

Advertisement