Damian Lillard sasa kuzeekea Blazzers

Sunday September 9 2018

 

NIPO sana tu. Ndivyo anavyopsema nyota wa mpira wa kikapu wa Ligi ya NBA, Damian Lillard ambaye alikuwa akiwindwa na Los Angeles Lakers.

Katika kuonyesha amedhamiria kuzeekea katika timu yake ya Portland Trail Blazzers na akiwa ndani ya mkataba unaoishia mwaka 2021, nyota huyo kaweka wazi kwa timu zilizokuwa zinamnyemelea, hana mpango wa kuchomoka kwenye timu hiyo na ameweka wazi malengo yake ni kuichezea timu hiyo maisha yake yote ya kucheza mchezo huo.

Nyota huyo ambaye alikuwa katika orodha ya wachezaji waliotajwa kucheza NBA All-Star mapema mwaka huu 2018, anasema wachezaji wengi wana kawaida ya kutamani kucheza timu tofauti tofauti na zaidi pale wanapohitajika na timu nyingine lakini kwake hilo halipo.

Aliongeza ameshakuwa na mapenzi na jiji lote la Portland, Jimbo la Oregon pamoja na watu wao na tamaduni zao jambo linalompa wakati mgumu kufikiria kuondoka na ikitokea akaondoka basi ni timu yenyewe iamue kumuuza kwa sababu za kibiashara.

Advertisement