Cristiano Ronaldo afunika saa ya mamilioni

Muktasari:

  • Juventus wanakutana na Manchester United kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya leo Jumanne. Ronaldo anakutana na timu yake zamani, huku Man United wakitarajia kupambana kwa kila namna ili kuhakikisha wanaibuka na ushindi. Mchezo huo utachezwa leo usiku.

 

Hispania. Nyota wa Juventus, Cristiano Ronaldo ameitambulisha saa ya gharama ambayo imetengenezwa kwa vito vya thamani, baada ya kuonyesha wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Saa hiyo ya gharama ilitambulisha jana Jumatatu ikiwa ni siku moja kabla ya mchezo utaoikutanisha Juventus dhidi ya Manchester United mechi ambayo inatarajiwa kuwa na ushindiani mkali kutokana na ubora wa timu hizo.

Timu hiyo za zamani ya Ronaldo, Man United itakuwa na kibarua kigumu cha kulinda heshima yake kwenye uwanja wao wa nyumbani ili kuhakikisha inaibuka na ushindi.

Saa ya Ronaldo inatajwa kuwa na thamani ya Dola 1.85 milioni huku ikiwa imenakshiwa vito vya madini ya thamani.

Ronaldo atashuka dimbani akiikabili timuyake ya zamani kwenye Kundi  H mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Old Trafford.

Nyota huyo wa  Juventus anakuwa mchezaji nyota mwingine duniani wenye majina makubwa kwenye tasnia ya soka akiwa na saa ya gharama.

Kwa mujibu wa Jarida la Forbes, linaeleza kwamba Bondia Floyd Mayweather ndiye mtu anayemiliki saa ya gharama ambayo inatajwa kuwa na thamani ya Dola 14 milioni.

Hata hivyo, Ronaldo anashuka dimbani leo huku akiandamwa na kashfa ya ubakaji inayomkabili kutokana na mashtaka  ya ubakaji ya mwanamitindo Kathryn Muyorga kwenye hoteli moja jijini Las Vegas, Marekani mwaka 2009.