Courtois awashangaa Chelsea kumkasirikia

Sunday September 9 2018

 

KIPA Thibaut Courtois amesema anahuzunishwa na namna mashabiki wa Chelsea walivyouchukulia kwa hasira uamuzi wake wa kwenda kujiunga na Real Madrid kwenye dirisha lililopita.

Wakati anajaribu kulazimisha uhamisho huo kufanyika, Courtois aligoma kwenda kwenye mazoezi ya Chelsea na jambo hilo liliwafanya mashabiki wa The Blues kujenga chuki dhidi yake.

Hata hivyo, kipa huyo Mbelgiji alisema mashabiki wa Chelsea wanapaswa kufahamu huo ni uamuzi wake wa kuondoka kwenye timu hiyo kuhamia Real Madrid, hivyo hawapaswi kuwa na hasira.

“Naamini mambo yatabadilika. Watu wasione nimeona hakuna viwango vya kutosha huko Chelsea, sikuwa na maana hiyo. Sisemi Chelsea haina kiwango, ule uhamisho ulikuwa muhimu kwangu,” alisema.

“Nafahamu kuna mashabiki wengine wa Chelsea watanielewa kwenye uamuzi huu niliochukua. Nawatakia kila la heri na nimefurahi kwa ushindi wao wa mechi nne za mwanzo kwenye Ligi Kuu England na waendelee hivyo hadi wabebe ubingwa.”

Advertisement