Barcelona yashikilia kibarua cha kocha Real Madrid

Muktasari:

  • Real Madrid leo itakuwa na kibarua kigumu mbele ya timu ya Crez ya  Viktoria Plzen kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hii inaweza kuwa ni habari mbaya kwa Kocha wa Real Madrid, Julen Lopetegue  baada ya kuwapo tetesi kuwa huenda Antonio Conte akarithi mikoba yake.

Miamba hiyo ya soka barani Ulaya imepoteza michezo yake ya mwisho minne kati ya mechi tano.

Pia Real Madrid inakamata nafasi ya saba kwenye msimamo wa La Liga baada ya juzi Jumapili kupoteza mchezo wake ilipokutana na dhidi ya Levante mechi ambao iliiisha kwa Real Madrid kuzamishwa mabao 2-1.

Kutokana na mfululizo wa matokeo hayo mabaya, tayari kumekuwa na minong’ong’ono kuwa huenda Conte akarithi mikoba ya kocha huyo kipindi cha kiangazi.

Matokeo mabaya ya Jumapili yameiweka pabaya Real Madrid kuelekea mchezo dhidi ya mahasimu wao Barcelona Jumapili wiki ijayo.

Kwa mijibu wa Gazeti la The Mirror, hadi sasa Conte ndiye kocha pekee anayetajwa kuwa ana asilimia kubwa kuchukua mikoba ya Popetegui ambaye kibarua chake ni hatihati kuendelea.