Mahrez abakiza hatua chache tu kutua Man City

Sunday July 8 2018

 

WINGA wa Leicester City, Riyad Mahrez yupo kwenye hatua za mwisho kabisa kukamilisha uhamisho wake wa kwenda kujiunga na Manchester City.

Kumekuwa na ugumu kidogo kwa Leicester kumruhusu supastaa wao huyo matata kabisa kwenda kujiunga na wapinzani wao kwenye Ligi Kuu England.

Leicester ilihitaji ilipwe Pauni 80 milioni kwa ajili ya huduma ya Mahrez wakati Man City walipopeleka ofa ya kumsajili kwenye dirisha la Januari, lakini walibadili mawazo baada ya kukutana na jambo hilo.

Lakini, kwa sasa mambo yanaonekana kwamba yanaweza kwenda vizuri na dili hilo kukamilishwa kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi na kwamba kocha Pep Guardiola anaweza kupata huduma ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Algeria kwa ada ya Pauni 60 milioni tu.

Bado kuna makubaliano machache sana hayajakamilika, lakini pande zote zinaonekana kuwa tayari kumaliza biashara hiyo

Advertisement