Emery kuleta mashine inaitwa Adrien Rabiot

Friday December 7 2018

 

LONDON, ENGLAND. UKIKICHEKI kikosi cha Arsenal kipo bomba kinoma. Lakini, Kocha Unai Emery bado anaona kuna sehemu ina mapengo na amepanga kushusha mashine ya maana huko Emirates.

Kutokana na hilo, Kocha Emery sasa amepanga kumnasa kiungo wa PSG, Adrien Rabiot, ambaye alifanya naye kazi huko Paris kabla ya kutumkia zake Emirates kwenda kuchukua mikoba ya Arsene Wenger.

Emery alifanya kazi na Rabiot kwa misimu mwili huko PSG na kocha huyo hakika ni shabiki mkubwa wa kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa. Kutokana na mpango wa Aaron Ramsey kuondoka kwenye timu hiyo, Rabiot anatazamwa kama mrithi wake.

Ripoti zilizotolewa na Calciomercato.com zinadai Arsenal ipo kwenye mazungumzo na Mama wa Rabiot, Veronique, kuhusu mpango wa kumnasa kiungo huyo ili akakapige London. Rabiot anaweza kusaini mkataba wa awali wa kujiunga na Arsenal ni Januari Mosi, mwakani.

Advertisement