WR2018: Wokorach wa Uganda 7s aihofia Samoa Kombe la Dunia Raga

Muktasari:

  • Uganda 7s, maarufu kama Cranes, imepangiwa kukutana na Samoa leo katika hatua ya mtoano ya michuano hii na Wokorach anasema ili waweze kufikia malengo yao ni lazima waifunge Samoa, ambapo mshindi wa mechi hii atakutana na England katika hatua ya 16 bora.

San Francisco. Winga wa timu ya taifa ya mchezo wa Raga ya Uganda 7s, anayekipiga katika klabu ya Kabras Sugar, Philip Wokorach anaamini huu mwaka wa Uganda kufanya maajabu katika michuano ya Kombe la Dunia, yanayoanza leo, lakini kikwazo kikubwa ni Samoa.
Uganda 7s, maarufu kama Cranes, imepangiwa kukutana na Samoa leo katika hatua ya mtoano ya michuano hii na Wokorach anasema ili waweze kufikia malengo yao ni lazima waifunge Samoa, ambapo mshindi wa mechi hii atakutana na England katika hatua ya 16 bora.
Uganda ambao wanajivunia kushinda Ubingwa wa Afrika mara mbili pamoja na kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye makala ya nne ya michezo ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika Aprili mwaka huu, wanashiriki Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza baada ya kipindi kirefu.  


 Kikosi cha Uganda 7s
1. Desire Ayera, 2. Timothy Kisiga, 3. Aaron Ofoyrwoth, 4. Pius Ogena, 5. Byron Oketayot, 6. Adrian Kasito, 7. Solomon Okia, 9. James Odongo, 9 Michael Okorach, 10. Justin Kimono, 11. Philip Wokorach, 12. Ivan Magomu

Ratiba ya Kombe la Dunia 2018
Ijumaa, Julai 20, mtoano:

Saa 5.01 usiku, Kenya vs Tonga
Saa tano 5.23 usiku, Canada vs Papua New Guinea
Saa 5.45 usiku France vs Jamaica
Saa 6.07 usiku, Wales vs Zimbabwe
Saa 6.29 usiku, Samoa vs Uganda
Saa 6.51 usiku, Russia vs Hong Kong
Saa 7.13 usiku, Japan vs Uruguay
Saa 7.35 usiku, Ireland vs Chile


Jumamosi, Julai 21, hatua ya 16 bora
Saa 11.03 asubuhi, Scotland vs (Kenya/Tonga)
Saa 11.25 asubuhi Argentina vs (Canada/Papua New Guinea)
Saa 11.47 asubuhi Australia vs (France/Jamaica)
Saa 12.09 asubuhi England vs (Samoa/Uganda)
Saa 12.31 asubuhi New Zealand vs (Russia/Hong Kong)
12.53 asubuhi Fiji vs (Japan/ Uruguay)
1.15 asubuhi Afrika Kusini vs (Ireland/Chile)
1.37 asubuhi USA vs (Wales/ Zimbabwe)