WR2018: Kenya na Uganda watupwa nje, Kombe la Dunia mchezo wa Raga

Saturday July 21 2018

 

By Fadhili Athumani

San Francisco, Marekani. Wawakilishi wa Afrika mashariki, Kenya na Uganda wameyaaga mashindano ya Kombe la Dunia ya Mchezo wa Rugby, yaliyoingia siku ya pili Jijini San Francisco,i Marekani, baada ya kushindwa kufurukuta mbele ya Scotland na Samoa jana.
Kenya ilianza vizuri na kutinga hatua ya 16, wakiwatoa Tango katika hatua ya mtoano kwa ushindi wa trai 19-7, wenzao Uganda wakijikuta wakibatizwa kwa moto na kutoka mapema tu, baada ya kulimwa 45-7 na wababe Samoa.
Baada ya hapo, majira ya saa 11.03 alfajiri ya leo, Shujaa inayonolewa na Innocent Simiyu walijitosa uwanjani wakiwa na matumaini makubwa ya kutinga robo fainali, lakini walijikuta ndoto zao zikizimwa na Scotland, walipotandika 26-31.
Kenya walianza vyema mchezo huo, ambapo hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, walikuwa wanaongoza 26-0 na kuonekana ni kama wameshavuka lakini kumbe akili za Waskochi zilikuwa zinawaza tofauti ambapo katika kipindi cha pili, waliweza kurudisha trai zote na kumalixa mchezo wakiwa kifua mbele 26-31 na hiyo ikawa mwisho wa safari ya Kenya.
Kwa matokeo hayo, Scotland wamesonga mbele kuingia hatua ya robo fainali ambapo watakutana na mshindi kati ya Afrika Kusini na Ireland huku Kenya wao wakisubiri kucheza mechi ya 'best looser' ambapo watachuana timu itakayooteza katika mchezo wa Afrika Kusini dhidi ya Ireland.

Advertisement