WR2018: Kenya 7s kutikisa San Francisco

Friday July 20 2018

 

By Fadhili Athumani

San Francisco. Zikiwa zimesalia saa chache wajitose uwanjani kusaka ubingwa wa Dunia, katika michuano ya Kombe la Dunia 2018, yanayoanza leo huko San Francisco nchini Marekani, timu ya taifa ya Kenya ya mchezo wa Raga, Kenya 7s wametamba kufanya makubwa.
Kenya wanashuka dimbani kuanzia saa tano usiku kukipiga dhidi ya Tonga, na Kocha wa Shujaa, Innocent Simiyu anaamini kikosi chake, kilichowasili mjini San Francisco siku ya Jumatatu, kina uwezo wa kufanya vizuri kwenye michuano tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.
"Maandalizi yamekamilika, vijana wako vizuri sana. Hali ya hewa imetulia sana, Jumanne tulifanya mazoezi mepesi, baadae tukaenda Gym, leo tunaingia uwanjani tukiwa na morali, nadhani tutarajie habari nzuri," alisema Simiyu.


Ratiba ya Kombe la Dunia 2018
Ijumaa, Julai 20, mtoano:

Saa 5.01 usiku, Kenya vs Tonga
Saa tano 5.23 usiku, Canada vs Papua New Guinea
Saa 5.45 usiku France vs Jamaica
Saa 6.07 usiku, Wales vs Zimbabwe
Saa 6.29 usiku, Samoa vs Uganda
Saa 6.51 usiku, Russia vs Hong Kong
Saa 7.13 usiku, Japan vs Uruguay
Saa 7.35 usiku, Ireland vs Chile

Jumamosi, Julai 21, hatua ya 16 bora
Saa 11.03 asubuhi, Scotland vs (Kenya/Tonga)
Saa 11.25 asubuhi Argentina vs (Canada/Papua New Guinea)
Saa 11.47 asubuhi Australia vs (France/Jamaica)
Saa 12.09 asubuhi England vs (Samoa/Uganda)
Saa 12.31 asubuhi New Zealand vs (Russia/Hong Kong)
12.53 asubuhi Fiji vs (Japan/ Uruguay)
1.15 asubuhi Afrika Kusini vs (Ireland/Chile)
1.37 asubuhi USA vs (Wales/ Zimbabwe)

Advertisement