Migne aifuata Harambee Stars India

Friday June 1 2018

 

Nairobi. Hatimaye Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’, Sebastien Migne na makocha wenzake, wameondoka nchini leo kuelekea nchini Indiakuungana na kikosi hicho kinachojiandaa na mashindano ya Intercontinental.

Migne na kocha msaidizi Nicolas  Bourriquet-cor, kocha wa makipa, Guilaune Coffey na kocha wa viungo, Osteopath Ludovic Breul walishindwa kuongozana na kikosi cha Stars, kutokana na kuchelewa kwa Visa zao, kwa kile kilochoelezwa kuwa ni kutotimia kwa baadhi ya masharti.

Msafara wa kwanza wa Stars, uliondoka nchini Jumatano iliyopita, ukiongozwa na Francis Kimanzi, aliyesimamia kikosi hicho kwa niaba ya Migne.

Beki wa Thika United, Dennis Odhiambo na nyota wa Vihiga United, Bernard Ochieng pia waliondoka na Migne kuelekea India.

Harambee Stars wataanza kampeni yao kwenye michuano hiyo kesho dhidi ya New Zealand, kabla ya kukabiliana na wenyeji India katika mchezo wao wa pili (Juni 04). Juni 08, Stars watavaana na Chinese Taipei kwenye mchezo wao wa tatu.

Kikosi cha Harambee Stars:

Advertisement

Makipa: Timothy Odhiambo (Ulinzi Stars), Patrick Matasi (Posta Rangers), Bryne Omondi (Tusker)

Mabeki: Jockins Atudo (Posta Rangers), Musa Mohammed (hana timu), Michael Kibwage (AFC Leopards), Bernard Ochieng (Vihiga United), Dennis Odhiambo (Thika United), Johnstone Omurwa (Mathare United), Bolton Omwenga (Kariobangi Sharks), Erick Ouma (KF Tirana)

Viungo: Kenneth Muguna (KF Tirana), Vincent Wasambo (Kariobangi Sharks), Patillah Omotto (Kariobangi Sharks), Chrispin Oduor (Mathare United), Clifton Miheso (Buildcon FC), Duncan Otieno (AFC Leopards)

Washambuliaji: Ovella Ochieng (Kariobangi Sharks), Timothy Otieno (Tusker FC), John Makwatta (Buildcon FC) na Pistone Mutamba (Wazito FC)

Advertisement