Kenya yaanza Paris 7s, kwa Kishindo

Saturday June 9 2018

 

By Fadhili Athumani

Nairobi, Baada ya kuinyanyasa mara mbili msimu huu, kwenye msururu wa HongKong na Singapore, hatimaye Kenya imefanikiwa kulipa kisasi dhidi ya Fiji kwa kuitandika 22-19, kwenye mchezo wa pili wa kundi A, uliomalizika muda mfupi, Jijini Paris.


Katika mechi hiyo iliyoanza majira ya saa 8.46, Shujaa ilikuwa inahitaji ushindi ili kujihakikishia nafasi ya kuendelea kusaka ubingwa wa taji kuu la Paris 7s, baada ya kuangukia pua dhidi ya New Zealand katika mchezo wao wa kwanza uliopigwa saa 5.18 asubuhi.
Aidha, katika ushindi huo, Kenya hawakulipiza kisasi tu dhidi ya vinara hao wa msimamo wa Raga duniani, lakini pia walifanikiwa kuitoboa timu hiyo ambayo ilikuwa inajivunia kucheza mechi 26 bila kupoteza, msimu huu.


Vijana wa Innocent Simiyu walianza kwa kasi ya ajabu na kuongoza 15-0, kupitia trai za Collins Injera, Willy Ambaka na Andrew Amonde ambapo hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, Kenya ilikuwa inaongoza 15-7 baada ya Fiji kujibu mapigo kupitia kwa trai ya Semi Kunatani iliyomaliziwa na Nacuqu.
Trai ya Eric Ombasa, iliyomaliziwa na Eden Agero, ilipanua wigo wa ushindi hadi 22-7 lakini Fiji waliamka na kuwashambulia Kenya ambapo  walifanikiwa kuandikisha trai mbili za haraka kupitia kwa Vakurunabili na Kalione Nasoko.

Hadi mechi inamalizika matokeo yalikuwa 22-19.Kenya itamaliza udhia na Samoa katika mechi za makundi.
Mechi hii itarindima kuanzia saa 1.52 usiku. Fiji ambayo inahitaji kushinda msururu wa Paris 7s I'll watawazwe mabingwa wa msimu huu wa HSBC World Sevens Series, watakutana na New Zealand. Mechi hii itaanza saa 2.14 usiku.


Matokeo kamili:
Australia 29-10 Wales
Ireland 14-5 Spain
Canada 33-10 Russia
South Africa 12-14 Scotland
New Zealand 24-5 Kenya
Fiji 35-12 Samoa
USA 26-7 Argentina
England 28-21 France

Australia 10- 17 Spain
Ireland 19-19 Wales
Canada 26-14 Scotland
South Africa 21-19 Russia
New Zealand 22 Samoa 17
Fiji 19-22 Kenya

Advertisement