Kenya yaitandika Equatorial Guinea

Monday May 28 2018

 

By Fadhili Athumani

Nairobi. Hatimaye kocha wa Harambee Stars, Sebastien Migne amepata sababu ya kukenua baada ya kikosi chake kuibuka na ushindi mwembambwa wa bao 1-0 dhidi ya Equatorial Guinea.
Huo ni ushindi wa kwanza kwa kocha Migne  katika michezo yake mwili tangu alipochukua jukumu la kuiongoza Stars kuitandika Equatorial Guinea katika mchezo wa kirafiki uliomalizika muda mfupi uliopita, kwenye Uwanja wa Kenyatta, mjini Machakos.
Bao pekee la ushindi lilipatikana katika dakika ya 72, kupitia kwa Piston Mutamba aliyeunganisha vyema krosi ya Whyvonne Isuza na kuamsha shangwe uwanjani hapo. Hadi kipyenga cha mwisho, Kenya wakatoka kifua mbele kwa 1-0 dhidi ya Equatorial Guinea.
Hata hivyo, kunako dakika ya 27, kituko cha aina take ulishuhudiwa uwanjani hapo baada ya mwamuzi wa mchezo kuamua kumlima kadi ya njano mchezaji wa Equatorial Guinea, wakati ikidhaniwa kuwa kachezewa rafu.
Mchezaji Bassilo Ndom, alianguka ndani ya boksi ya Kenya, baada ya kukwatuliwa na beki wa Stars, Joash Onyango, lakini kwa mshangao wa wengi mwamuzi akaamua kumuadhibu Ndong na kuwanyima Equatorial Guinea penalti.
Mfaransa huyo, anayesaidiwa na wakufunzi wa U19 na U20, Francis Kimanzi na Stanley Okumbi, anatumia mechi hizo mbili za kirafiki kama sehemu ya maandalizi kabla ya kukutana na Ghana katika mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu michuano ya mataifa huru barani Afrika 2019.


Kikosi cha Stars:
Patrick Matasi,  Joackins Atudo , Philemon Otieno , Musa Mohammed ,  Joash Onyango , Erick Ouma, Duncan Otieno , Whyvonne Isuza , Francis Kahata , Kenneth Muguna , Pistone Mutamba
Akiba: Bonface Oluoch , Timothy Odhiambo , Timothy Omwenga , Harun Sharkava , Jafari Owiti ,  Chrispine Oduor , Humphrey Mieno , Ovella Ochieng , Patillah Omotto, Mike Kibwage , Otieno Omurwa


Equatorial Guinea

Felipe Ovono,  Federico Obana, Cosme Anvene, Fernando Rui Da Gracia, Esteban Orozco, Valeriano Nchama, Federico Bicoro, Pablo Ganet, Iban Salvador, Nicolas Kata Senga,  Basilio Ndong
Akiba: Pascacio Ebea, Pensy Achille, Luis Enrique Nsue,  Mariano Ondo,  Benjamin Edu Ndong,  Saul Coco Bassey, Pedro Asu Mbengono

Advertisement