annesa, Tiwa Savage wanogesha Siku ya Wanawake Duniani

Muktasari:

Boomplay pia itakuwa na kampeni kabambe ambayo itatoa fursa ya kukuza mauzo ya kazi za wanawake ambao nyimbo zao zitakuwepo kwenye playlist ya BOOM QUEENS, Playlist hiyo itakuwa na nyimbo za wasanii bora wa kike tu.

Siku ya Wanawake Duniani hapa nchini inaadhimishwa kitofauti na Boomplay kwa kuanzisha kampeni ya Boom Queens kwa kushirikiana na wasanii wa kike.

Vanessa Mdee, Rihanna, Tiwa Savage, Fena Gitu na wengine wengi, ni miongoni mwa wanawake wenye vipaji ambao wameendelea kubadilisha tasnia ya muziki duniani. App ya Boomplay itakuwa na muonekano wa tofauti hasa katika Siku ya Wanawake duniani tarehe 8 Machi, lengo likiwa ni kuonesha na kukuza kazi za wanawake katika muziki. App itapambwa na nyimbo, albamu pamoja na playlist za wanawake katika vipengele vyote kwenye ukurasa wa kwanza.

Boomplay pia itakuwa na kampeni kabambe ambayo itatoa fursa ya kukuza mauzo ya kazi za wanawake ambao nyimbo zao zitakuwepo kwenye playlist ya BOOM QUEENS, Playlist hiyo itakuwa na nyimbo za wasanii bora wa kike tu.

Katika kampeni hii, Meneja Mahusiano wa kampuni ya Boomplay, Bi Tosin Sorinola alisema, majadiliano juu ya usawa wa kijinsia ni moja ya mambo ambayo ni muhimu kwao kama jukwaa lenye nia kubwa ya kukuza wanawake katika muziki.

"Katika njia njema kadri iwezekanavyo. Kampeni hii sio kwa mara moja tu, ni endelevu, na hili litadhihirishwa katika shughuli zetu za kila siku”, alisema.