Ziyech kutua Chelsea mwishoni mwa msimu

Friday February 14 2020

Ziyech kutua Chelsea mwishoni mwa msimu,KOCHA wa Ajax, Erik ten Hag ,Hakim Ziyech

 

KOCHA wa Ajax, Erik ten Hag amesema staa wa timu hiyo, Hakim Ziyech atakuwa mchezaji wa Chelsea msimu ujao.

Winga huyo wa kimataifa wa Morocco ameripotiwa kukubali dili la kujiunga na Chelsea kwa ada ya Pauni 38 milioni na atakwenda kujiunga na timu yake mpya mwishoni mwa msimu huu.

Chelsea iliifukuzia saini ya staa huyo wa zamani wa Heerenveen na FC Twente kwenye dirisha la Januari baada ya kufunguliwa kutoka kwenye adhabu ya kufungiwa kusajili, lakini Ajax iligoma kumwaachia Ziyech katikati ya msimu ikisubiri hadi msimu umalizike. Kocha wa Ajax, Ten Hag alisema uhamisho huo upo kwenye hatua nzuri na ungetokea mapema zaidi.

Ten Hag alisema uhamisho wa Ziyech kwenda Chelsea ni jambo linalotarajia kwenda kutokea mwishoni mwa msimu.

Advertisement