Ziyech ‘ajivunja’ awahi England kukipiga Chelsea

London, England. Hakim Ziyech amejiondoa katika kikosi cha Morocco ili kupata nafasi ya kujiandaa na mechi za Chelsea wikiendi hii.

Kiungo mshambuliaji huyo mbunifu alitua Chelsea akitokea Ajax na Blues na tangu kukamilika kwa usajili wake Februari hakuichezea timu yake mpya.

Lakini Ligi Kuu ikitarajiwa kuendelea tena wiki hii, Ziyech, ambaye sasa ana miaka 27, aliumia goti wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Brighton.

Alianza mazoezi kabla ya mapumziko ya kupisha timu za taifa, licha ya kocha Frank Lampard kusisitiza kuwa hajawawa fiti kuitumikia Blues.

Ziyech aliitwa na Morocco kwa ajili ya michezo ya timu ya taifa, licha ya Chelsea kuwa na makubaliano na RMFF.

Pande zote mbili zilikubaliana kwamba itakuwa vizuri kwa Ziyech kuwa benchi kwa muda katika mchezo wa Morocco dhidi yaSenegal uliofanyika Ijumaa, kabla ya kachana na mchezo wa mwisho na kurudi Cobham.

Aliingia dakika ya 31 mjini Rabat, akitoa pasi ya bao wakati Morocco ikishinda 3-1 dhidi yaTeranga.

Ziyech atakosa mchezo wa kirafiki wa taifa lake dhidi ya DR Congo kesho.

Anatarajiwa kuwamo katika mchezo ujao wa Chelsea itakayoialika Southampton kwenye Uwanja wa Stamford Jumamosi ijayo.

Mchezaji ambaye hatakuwepo ni kipa aliyenunuliwa kwa Pauni 22 milioni, Edouard Mendy.

Nyota huyo wa miaka 28 alitakiwa kumvaa Ziyech na Morocco yake dhidi ya Senegal, lakini aliumia katika mchez uliopita.