Zidane kumbakiza Hazard Chelsea

Muktasari:

Hazard amekuwa na ndoto ya siku moja kufanya kazi na Zidane ambaye anatajwa atachukua nafasi ya Sarri kama atatimuliwa muda wowote na bilionea wa klabu hiyo Roman Abramovich.

London, England. Nyota wa Chelsea, Eden Hazard ameanza huenda akabaki Stamford Bridge, kama Zinedine Zidane atapewa mikoba ya Maurizio Sarri.

Mtaliano Sarri amekalia kuti kavu Chelsea kutokana na kipigo cha aibu cha mabao 6-0 ambacho timu yake ilikutana nacho siku chache zilizopita kutoka kwa Manchester City.

Miongoni mwa vyombo vya habari nchini England, vimeandika kuwa kuna kila dalili za Hazard kufikiria upya uamuzi wake wa kutaka kuondoka kwenye klabu hiyo.

Hazard amekuwa na ndoto ya siku moja kufanya kazi na Zidane ambaye anatajwa atachukua nafasi ya Sarri kama atatimuliwa muda wowote na bilionea wa klabu hiyo Roman Abramovich.