Zidane anakuja Old Trafford

Muktasari:

Ingawa taarifa makamo mwenyekiti wa Manchester United Ed Woodward yupo katika kikao cha ana kwa ana na Jose Mourinho jijini London, taarifa zimefichua kuwa siku za Mourinho kubaki Old Trafford zinahesabika kwa kuwa mipango ya kumpa mikoba Zinedine Zidane imekamilika.

London, England. Ingawa kikao kinachoaminika cha kuzima bifu kinaendelea jijini London, kati ya makamo mwenyekiti wa Manchester United, Ed Woodward na kocha Jose Mourinho, siri imevuja kuwa kocha huyo anapumbazwa.

Wakati kikao hicho kikiendelea siri imevuja kuwa Mourinho ana asilimia ndogo ya kuendelea kubaki Old Trafford kwani mipango ya kumtwaa Zinedine Zidane, imekamilika na sasa sio tetesi tena.

Zidane alikuwa London kwa wiki kadhaa na familia yake katika kilichoelezwa kuwa mapumziko ya kawaida lakini kumba alikua akikamilisha mazungumzo na mabosi wa United.

Matokeo yasiyoridhisha ya timu, kukwaruzana na Woodward na kiungo Paul Pogba kumechangia United kufikiria kumtosa Mourinho, Kwa mujibu wa kiungo wa zamani wa United, Paul Ince.

Kiungo huyo aliyekuwa mkorofi enzi zake alisema siku za Mourinho kuaga ninahesabika na kwamba dakika yoyote Zidane atatangazwa kocha mpya wa United.

Alisema bila shaka bodi ya United inasubiri saa itimie tu iweze kumtangaza Zidane kuchukua timu kutokana na kukatishwa tamaa na mwenendo wa timu na namna Mourinho anavyokwaruzana kila mara na wachezaji wake.

Ince alisema kuwa mfumo aliokuwa akiutumia Zidane katika Real Madrid unaendana kwa kiasi kikubwa na uliopo United, hivyo wana matarajio makubwa kuwa mfaransa huyo atawapa ufanisi tofauti na hali ilivyo kwa sasa.

Pogba mchezaji ghali Duniani am eshasema mara kadhaa kuwa anahitaji kuondoka Old Trafford kwenda Barcelona kwa sababu ya kukosa furaha.

Mbali ya kauli ya Ince, pia kuna taarifa zimevuja kuwa mshambuliaji Romelu Lukaku aliridhia ofa ya kujiunga na mabingwa wa Ligi Kuu Italia, Juventus lakini amesitisha shinikizo baada ya kuthibitishiwa kuwa Zidane atatua Old Trafford.

Kakake Lukaku, aitwaye Jordan, ambaye anakipiga Lazio amefichua taarifa hizo za mshambuliaji huyo wa kibelgiji kutakiwa na Juventus.