Zidane ampa presha Mourinho

Tuesday September 11 2018

 

ZINEDINE Zidane ameripotiwa kuzidi kumtia presha Jose Mourinho na kibarua chake huko Manchester United baada ya Mfaransa huyo kudai yupo mbioni kurudi kazini.

Zidane kwa sasa hana timu tangu alipoachana na Real Madrid mwishoni mwa msimu uliopita na jina lake limekuwa likitajwa sana likihusishwa na kibarua cha kwenda kuinoa Man United, hivyo kwa kauli yake ya kusema atarudi kazini hivi karibuni, inampa wasiwasi Mourinho, huenda kuna mtu anakuja kuchukua kibarua chake kimyakimya.

Zidane ameondoka Real Madrid baada ya kuipata mataji matatu mfululizo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Advertisement