Zayd ana siri za Mbwana Samatta

Tuesday January 8 2019

 

By Olipa Assa

ZINAHESABIKA siku tu kabla ya Yahya Zaidi kuuzwa na klabu yake ya Azam kwa Ismaily ya Misri, lakini mwenyewe amefichua tangu aanze kutamba amekuwa akitembea na siri ya mafanikio ya Mbwana Samatta anayekipiga KRC Genk ya Ubelgiji.

Zayd aliliambia Mwanaspoti akiwa timu ya vijana za Azam ndoto yake ilikuwa kucheza Ligi Kuu Bara, baada ya kufanikiwa, akaanza kuwaza anga za Samatta ambaye ana mafanikio makubwa ndani na nje ya nchi.

“Nina malengo ya kucheza nje na mchezaji ambaye alinipa changamoto zaidi ni Shaaban Idd ‘Chilunda’ baada ya kufanikiwa kutoka kabla yangu, nilijipa moyo, niliongeza juhudi katika kazi nikiamini kuna siku itakuwa zamu yangu,” alisema. “Mimi ni muumini wa nidhamu kwa kujifunza kutoka wa walionitanguliwa kama nahodha Aggrey Morris, John Bocco ambaye nilikuwa napenda anavyopambana uwanjani nilikuwa namfuata ili anielekeze na alifanya hivyo, huku nikitamani kufika mbali kama Samatta jinsi alivyofanikiwa.”

Advertisement