Zahera ammwaga Mkongo

Muktasari:

  • Uamuzi huo uliwashtua mabosi wa Yanga na hata walipojaribu kumhoji zaidi kocha huyo alisimama katika msimamo wake akisema hataki mchezaji wa kigeni anayehitaji kutengenezwa zaidi.

KAMA ni kocha Yanga imempata, kwani Mwinyi Zahera hataki masihara na kazi yake na unaambiwa kama utani ameamua kumchomoa winga wake mpya hata kabla ya kuvaa uzi wa klabu hiyo.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinasema, yule winga Ruben Bomba amemtibua Zahera baada ya kumshtukia kwamba kwa sasa hayupo katika ubora aliomuacha nao akiwa kwao DR Congo.

Bomba aliletwa na Zahera lakini baada ya kuanza mazoezi wiki iliyopita Zahera hakukubaliana na ubora wake na kuwaambia mabosi wa klabu yake hakuna dili la winga huyo tena.

Uamuzi huo uliwashtua mabosi wa Yanga na hata walipojaribu kumhoji zaidi kocha huyo alisimama katika msimamo wake akisema hataki mchezaji wa kigeni anayehitaji kutengenezwa zaidi.

Bosi mmoja wa Yanga amesema Zahera amewaambia mabosi wake kuwa Yanga haihitaji mchezaji anayekuja kutengenezwa zaidi hasa akiwa wa kigeni na kwamba Bomba uwezekano wa kusajiliwa ni asilimia 2% lakini kutosajiliwa ni asilimia 98%.

“Kocha ameshindwa kukubaliana na kiwango cha Bomba na ni yeye alimleta hapa lakini katika taarifa yake na viongozi wenzetu wa usajili anasema Bomba aliyemuacha kwao sio huyu wa sasa ameshuka sana,”alisema