Zahera afumua kiungo Yanga

Muktasari:

Yanga inaanza hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika wakiwa nyumbani dhidi ya Zesco ya Zambia,mchezo utakaopigwa masaa machache yajayo Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amefumua ukuta na kujaza viungo katika kikosi chake kitakachoshuka uwanjani kuwavaa Zesco
Katika kikosi hicho Zahera ameanza na kipa mzawa Metacha Mnata golini huku Mkenya Farouk Shikhalo akianzia benchi.
Katika ulinzi ingizo jipya ni Mapinduzi Balama kurudishwa kucheza kama beki wa kulia akichukua nafasi ya Paul Godfrey 'Boxer'aliyeumia.
Walinzi wa kati wameendelea kuwa Lamine Moro na Kelvin Yondani huku beki wa kushoto ikibaki wa Ally Mtoni  'Sonso.
Katika kiungo Zahera amemuingiza mtu mpya Abdulaziz Makame akicheza kiungo cha chini sambamba na Feisal Salum 'Fei toto wakisaidiana pia na Mohamed Issa 'Banka' atakayekuwa anatokea kulia
Faida kubwa kwa safu hiyo ni kutokana na viungo wote hao kujuana vyema hata kama wanacheza pamoja katika kikosi cha Yanga kwani viungo hao ndiyo viungo katika kikosi cha Zanzibar Heroes.
Makame sasa anakuwa amemuhamisha namba nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi ambaye atacheza nyuma ya mshambuliaji wa mwisho sambamba na Sydney Urikhob huku winga ya kushoto ikibaki kwa Patrick Sibomana.
Katika benchi Zahera amewabakiza Shikhalo,mabeki Mharami Issa,Ally Ally,kiungo Deuse Kaseke na  washambuliaji Mrisho Ngassa, Juma Balinya na Maybin Kalengo.