Zahera: Yanga inabeba pointi tatu kwa Biashara

Muktasari:

Zahera alisema anatambua ugumu unaokuwepo kwa timu zilizopo mkiani jambo linalomfanya awaweke kitimoto wachezaji wake kutoidharau Biashara

KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera  hataki mchezo kabisa linapofika suala lá kukokotoa pointi katika mchezo wao wa Jumapili dhidi ya Biashara ameamua kupanga mkakati mzito kuhakikisha hawapotezi mchezo huo.
Zahera alisema anatambua ugumu unaokuwepo kwa timu zilizopo mkiani jambo linalomfanya awaweke kitimoto wachezaji wake kutoidharau Biashara kwa nafasi waliyopo.
 "Mechi yetu na Biashara ni ngumu sana kwetu kwasababu nafahamu changamoto ya kucheza na timu âmbayo ipo katika nafasi mbaya katika msimamo wa ligi nimewaambia wachezaji wangu kujiandaa kisaikolojia na kulichukulia kiumakini suala golo, "
"Itakuwa mechi nguvu saana na nitakua mkali sana kwa wachezaji wangu katika mechi hiyo ambayo ni muhimu sana kwetu kuendelea kuendeleza rekodi yetu ya kutokufungwa mchezo hata mmoja," aliena.
Alisema amewafuatilia sana wapinzani wao amegundua ni wazuri sana lakini kunavitu vinawakwamisha na ndio wanatarajia kutumia mapungufu hayo kuwafunga.