Zahera, Makambo watwaa Tuzo Ligi Kuu Bara

Friday December 7 2018

 

By Mwandishi Wetu

 Dar es Salaam. Kamati ya Tuzo imemchagua Kocha Mkongo wa Yanga, Mwinyi Zahera kuwa Kocha Bora wa Novemba pia mshambuliaji wake, Mwinyi Zahera akitwaa uchezaji bora.

Zahera amenyakua Tuzo hiyo akiwashinda Kocha Mkuu wa Coastal Union, Juma Mgunda na Kaimu Kocha Mkuu wa Alliance FC, Gilbert Dadi alioingia nao fainali.

Hii ni kutokana na klabu yake kufanya vizuri katika klabu zote 20, zinazoshiriki michuano hiyo na sasa wanaongoza Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 38, ikifuatiwa na Azam FC yenye 36, Simba 27, na Mtibwa Sugar iliyo ya nne na pointi 23.

Iko hivyo pia kwa mshambuliaji wake huyo, aliyemleta mwenyewe kutoka Congo na kuchaguliwa katika Tuzo hiyo. Makambo raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kama ilivyo kwa Zahera alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake Said Dilunga wa Ruvu Shooting na beki Abdallah Shaibu wa Yanga.

Advertisement