Zahera: Huyu Feisal aende TP Mazembe

Wednesday August 8 2018

 

By KHATIMU NAHEKA

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kama kuna usajili umemfurahisha ambao hakuulewa kabla basi ni kusajiliwa kwa kiungo Feisal Salum ‘Fei Totoo.

Akizungumza na Mwanaspoti Zahera alisema Feisal ni kiungo hodari na kwamba mabosi wa klabu hiyo wajiandae kumuuza mbali katika klabu kubwa Afrika.

Zahera alisema mpaka sasa hajajua ampange wap kiungo huyo katika nafasi za viungo kutokana na kumudu majukumu mengi anayompa.

Kocha huyo alisema kama kiungo huyo akicheza sambamba na Mkongomani Pappy Kabamba Tshishimbi pamoja na Mohamed Issa ‘Banka basi timu hiyo itakuwa na makali zaidi kuweza kumudu kukutana na yoyote.

Alisema dozi ya mazoezi ambayo Feisal anaipata sasa inazidi kumuongezea ubora mkubwa katika majukumu yake huku akiongeza akisema nidhamu yake iko juu wakati wote.

“Nimemuona Feisal ni mchezaji mdogo lakini kipaji chake kinaonekana kuzidi hata umri wake anajua san nafikiri tumepata mtu mali kwa hii klabu,” alisema Zahera.

“Nasubiri Banka ajiunge kama akicheza sambamba na Pappy,Feisal na Pappy basi tutakuwa na timu imara sana, ninachopenda zaidi nidhamu yake iko juu na kila kazi unayompa anaifanya kwa kiwango bora.”

Advertisement