Yoso azigonganisha England, Nigeria

Muktasari:

  • Wazazi wa mchezaji huyo wa Southampton ni raia wa Nigeria ingawa alizaliwa, Ireland na kukulia London. Kanuni zinamruhusu kuchagua moja kati ya nchi hizo tatu kuitumikia.

London, England. Kocha wa timu ya Taifa ya Ireland, Martin O’Neill, amesikitishwa na zuio la Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kwa kinda Michael Obafemi mwenye miaka 18.

Wazazi wa mchezaji huyo wa Southampton ni raia wa Nigeria ingawa alizaliwa, Ireland na kukulia London. Kanuni zinamruhusu kuchagua moja kati ya nchi hizo tatu kuitumikia.

Kinda huyo ameshindwa kufanya uamuzi kwa kuwa kila nchi inamshawishi aitumikie, ameitwa na Kocha wa Nigeria licha ya kucheza timu za vijana chini ya miaka 14, 17 za England. Ireland imemuita kwenye kikosi cha vijana chini ya miaka 19 kinachonolewa na O’Neill.