Yondani apata mtoto wa nne

Muktasari:

Beki wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani ameongeza familia baada ya mkewe Nancy kujifunga mtoto wa nne.

Dar es Salaam.Beki wa Yanga, Kelvin Yondani na mkewe Nancy wamebahatika kupata mtoto wa kiume leo.

Yondani ambaye hivi karibuni hakuwa na nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza na kuwaacha Mghana Lamine Moro na Said Makapu wakitamba.

Mtoto huyo anakuwa wanne kwa Yondani na mkewe Nancy katika familia yao.

"Yondani amepata mtoto mwingine katika familia yake. Huyo ni wa tatu kwa wanaume na wa nne kwa familia yake," alisema jamaa wa karibu wa Yondani.

Alisema, hata Yondani hakuwa vizuri sana kutokana na kuwa karibu na mkewe.

"Si unajua mama zetu hawa, bila uangalizi mambo yanaweza kuwa si mambo," alisema rafiki huyo wa Yondani.

Yondani ameongeza familia kwa mke wake huyo baada ya kuishi pamoja kwa zaidi ya miaka 15.