Yondani aibukia mazoezini Taifa Stars

Tuesday July 23 2019

 

By Thomas Ng'itu

Dar es Salaam. Licha ya kuchelewa kujiunga kambini na Yanga, beki Kelvin Yondani leo amefanya mazoezi na kikosi cha timu ya Taifa Tanzania kwenye Uwanja wa Boko Veterani, jijini Dar es Salaam.

Yondani tangu arejea nchini kutoka katika fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon 2019, Misri) beki huyo ameshindwa kujiunga na kikosi cha Yanga kambini Morogoro.

Hata hivyo, Yondani alikuwa ameumia katika mchezo dhidi ya Kenya na kufanya akose mechi ya mwisho ya Afcon dhidi Algeria, hakukuwa taarifa majeruhi hayo yatamweka nje kwa muda gani.

Katika mazoezi yaliyokuwa yanasimamishwa na kaimu kocha mkuu Stars, Ettiene Ndayiragije akisaidiana na Seleman Matola na Juma Mgunda beki Yondani alifanya mazoezi na wachezaji wote.

Katika siku ya pili ya kambi hiyo Stars inajianda kwa mchezo dhidi ya Kenya wa kufuzu kwa CHAN 2020 Cameroon utachezwa Agosti 27, jijini Dar es Salaam wachezaji wote walikuwepo isipokuwa wale waliokuwa na Simba nchini Afrika Kusini.

Wachezaji waliofanya mazoezi ya asubuhi Metacha Mnata, Idd Mobby, Masoud Abdallah 'Cabaye', Frank Domayo, Abdulaziz Makame, Boniphace Maganga, Ayoub Lyanga na Salim Aiyee.

Advertisement

Juma Kaseja, Kelvin Yondani, David Mwantika, Paul Godrey 'Boxer', Feisal Salum, Paul Ngalema, Idd Seleman 'Nado' na Salum Abuoubary ‘Sure Boy’.

Advertisement