Yanga yapishana na Everton

Muktasari:

Yanga wamekubali kuondolewa kwa mara ya pili katika hatua ya awali ya mashindano ya SportPesa.

Yanga wamekubali kufungwa mabao 3-2 dhidi ya Kariobangi Skarks katika mechi ya kwanza ya mashindano ya SportPesa Super Cup.
Kufungwa kwa Yanga kuna maana ya kwamba wametolewa katika hatua ya awali ya michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya tatu.
Yanga watakuwa wamepishana na Everton kwani bingwa wa michuano hii huwa anacheza na timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza.
Yanga wamekubali kuondolewa kwa mara ya pili katika hatua ya awali ya mashindano ya SportPesa.