Yanga yaoga Manoti

Saturday November 9 2019

 

By Thomas Ng'itu

WACHEZAJI wa Yanga wameendelea kuoga manoti kutoka kwa wadhamini wao GSM baada ya jana Ijumaa kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Ndanda.
bao la faulo lililopigwa na winga Patrick Sibomana, liliwafanya Yanga kutoka kifua mbele katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Nangwanda Sijaona.
GSM leo wametoa kitita cha Shilingi 10 Milioni kupitia kwa Afisa Muhamasishaji wa klabu hiyo, Antonio Nugaz ambaye alimkabidhi nahodha msaidizi Juma Abdul.
Baada ya kupokea pesa hizo, Juma Abdul alisema kwa pamoja yeye na wachezaji wenzake wanashukuru kupokea kitita hicho.
"GSM wamekuwa wakituahidi mara kwa mara kutupa zawadi hizi kama tukishinda, kwahiyo ni jambo zuri hili kwetu kwa wao kutimiza ahadi," alisema.
Yanga wamekuwa wakipewa kitita cha Shilingi Milioni 10 kutoka kwa wadhamini hao pindi wanapopata matokeo ya pointi tatu.

Advertisement