Yanga yamtega Tshishimbi

Muktasari:

Tshishimbi aliyesajiliwa mwaka juzi kutoka Mbabane Swallows ya eSwatini, amekuwa akizinguana na mabosi wake hao juu ya kusaini mkataba mpya

MABOSI wa Yanga wamemtega nahodha wao, Papy Tshishimbi wakimpa muda wa wiki mbili ili kuamua hatma yake klabuni hapo kwa kusaini mkataba mpya.

Tshishimbi aliyesajiliwa mwaka juzi kutoka Mbabane Swallows ya eSwatini, amekuwa akizinguana na mabosi wake hao juu ya kusaini mkataba mpya, ambapo Yanga ilimuwekea mzigo mezani ili asaini miaka miwili, huku yeye akitaka aongezewe.

Katika kutegeana huko, mabosi wa Yanga wameamua kumpa wiki mbili kiungo huyo fundi wa mpira ili kuhakikisha anatoa maamuzi ya mwisho kama kukubali mzigo na kusaini la sivyo asepe zake.

Katibu Mkuu wa Yanga, wakili Simon Patrick ameithibitishia Mwanaspoti kwamba kama watashindwa kufikia muafaka wa usajili mpya wa Tshishimbi hadi Jumatano ijayo basi wataachana naye rasmi na hakutakuwa na ukurasa mwingine wa staa huyo klabuni hapo.

Kauli ya Simon imekuja siku chache baada ya mchezaji huyo kutoafikiana na klabu hiyo juu ya usajili mpya kwenye dirisha kubwa baada ya kumaliza mkataba na klabu hiyo huku klabu ikitaka asaini miaka miwili na yeye akisisitiza kuwa dau walilompa ni la thamani yake kwa mwaka mmoja tu.

Je unajua kiwango cha fedha alichowekewa Tshishimbi na amesemaje juu ya hatma yake klabu hapo? Litafute Mwanaspoti la kesho Ijumaa Julai 31, 2020 upate majibu yote!