Yanga yajipanga kwa mechi nne Morogoro, Dodoma

Muktasari:

Yanga inaendelea kukisuka kikosi chake Morogoro tayari kwa Ligi Kuu, Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Dar es Salaam. Uongozi wa Yanga umesema unatarajia kucheza mechi nne za kirafiki kabla ya kushuka uwanjani kutambulisha wachezaji wake mapema mwezi ujao.

Yanga ipo kambini Morogoro inatarajia kucheza mechi za kirafiki kati ya Julai 15, 19, 23 na Agosti 3 mwaka huu.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Dismass Ten alisema michezo hiyo ni kwaajili ya kuimarisha zaidi kikosi chao ambacho wanaamini kitakuwa miongoni mwa vikosi shindani.

"Naamini michezo hiyo itatoa fursa kwa wakazi wa maeneo tutakayocheza kujionea usajili mpya tulioufanya kabla ya kilele cha siku ya Mwananchi jijini Dar es Salaam."

"Tunawaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kutupa sapoti hasa katika michezo hiyo ikiwa ni sambamba na kujionea usajili bora tulioufanya,"

"Julai 23 tutakuwa Dodoma ambapo tunatarajia kucheza na Dodoma FC katika uwanja wa Jamhuri wakazi wa huko wakae tayari kupokea timu," alisema Ten.