Yanga yaivaa Mtibwa Sugar bila Fei Toto, Yondan

Muktasari:

Kelvin Yondani ataukosa huo pia kutokana na kulimwa kadi nyekundu kwenye mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar jijini Mwanza.

Dar es Salaam. Kiungo wa klabu ya Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ na beki Kelvin Yondan wataukosa mchezo wa leo dhidi ya Mtibwa Sugar kutokana na kuwa na kadi.
Fei Toto ataikosa mechi hiyo ya leo Jumatano kutokana na kuwa na kadi tatu za njano ambazo kwa mujibu wa kanuni za soka hatakuwa sehemu ya wachezaji wa leo.

Simba, Yanga mtihani mgumu mechi za ugenini
Pia, Kelvin Yondani ataukosa huo pia kutokana na kulimwa kadi nyekundu kwenye mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar jijini Mwanza.

Wakati wawili hao wakikosekana, kikosi cha Yanga tayari kipo mkoani Morogoro tangu juzi kwa ajili ya maandalizi ya  mechi hiyo itakayoanza majira ya saa 8 mchana.

Yanga inayoongoza Ligi Kuu Tanzania Bara kwa pointi 74, itakuwa na kibarua kizito dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Rekodi inaonyesha kwa upande wa Yanga  inaweza kuibeba kwa kuwa tangu mwaka 2015 katika mechi nne ambazo timu hizo zimekutana imeshinda mara mbili, Mtibwa  mara moja na zimetoka sare moja.

Akizungumza kwa simu jana, Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera alisema Mtibwa ni timu bora ina kikosi chenye ushindani, lakini watapambana kupata pointi tatu.