Yanga yaanza kujenga ukuta

Saturday August 1 2020

 

By Khatimu Naheka

Yanga ambayo inafanya usajili wao kwa uwezeshaji wa wadhamini wao GSM leo Agosti Mosi, 2020 imekamilisha rasmi usajili wa beki wa kati Bakari Mwamnyeto akitokea Coastal Union.

Mwamnyeto amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga ambapo sasa anakwenda kuimarisha safu ya ulinzi ya timu hiyo.

Hatua ya usajili huo Yanga imewapiga bao watani wao Simba na hata Azam ambao walikuwa wakimpigia hesabu beki huyo ambaye amekuwa na msimu mzuri.

Wakati usajili wa Mwamnyeto ukikamilika wakafanya usajili mwingine wa beki wa kushoto Yassin Mustapha.

Mustapha amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga akitokea Polisi Tanzania aliyoitumikia msimu uliomalizika.

Ndani ya siku mbili Yanga imekamilisha usajili wa wachezaji watatu ambapo mapema jana kiungo wa Kagera Sugar Zawadi Mauya kisha leo wakafuata Mwamnyeto na Mustapha

Advertisement

Advertisement