Yanga yaanza Morrison, Molinga, Singida United yaingia Boban

Muktasari:

Kocha Luc Eymael wa Yanga ameanza washambuliaji wawili Bernard Morrison na David Molinga leo dhidi ya Singida United.

Singida. Mshambuliaji mpya wa Yanga, Benard Morrison ataanza pamoja na David Molinga katika mchezo wa leo dhidi ya Singida United kwenye Uwanja wa Liti, mjini Singida.

Kocha Luc Eymael ameamua kuwaanzisha washambuliaji wawili kwa lengo la kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo muhimu kwako baada ya kupoteza katika michezo miwili ya awali.

Mshambuliaji Morrison atakuwa akicheza mechi yake ya kwanza tangu alipojiunga na Yanga katika dirisha dogo msimu huu.

Pia kocha Eymael amemwanzisha kipa Metacha Mnata akichukua nafasi ya Faroukh Shikhalo, Said Makapu akicheza kama beki wa kati na Lamine Moto huku kiungo Papy Tshishimbi akirejea kikosini.

Wenyeji Singida United amemwanzisha kiungo wa zamani wa Yanga, Haruna Moshi ‘Boban’ kuongoza jahazi hilo huku kiungo Athuman Idd ‘Chuji akiwa benchi.

Boban na Mwakasega watakuwa na jukumu moja la kuhakikisha Singida United inaondoka na pointi tatu katika mchezo huo wa leo.

Vikosi;

Singida United: Owen Chaima, Aaron Lulambo, Haji Mwinyi, Daud Mbweni, Tumba Lui, Erick Mambo, Kazungu Mashauri, George Sangija, Elnyesya Sumbi, Haruna Moshi 'Boban' na Six Mwakasega.

Yanga;Mechata Mnata, Juma Abdul, Jafary Mohammed, Lamine Moro, Saidi Makapu, Pappy Tshishimbi, Deus Kaseke, Haruna Niyonzima, David Molinga, Bernard Morrison na Balama Mapinduzi.