Yanga ya Zahera yatumia CD kuisoma Alliance

Muktasari:

  • Zahera tunawaheshimu Alliance na tunatarajia kutumia CD kuwafuatilia katika baadhi ya michezo waliyocheza ili kutambua mapungufu yao.

Dar es Salaam. Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema anawaheshimu Alliance na anatarajia kukaa na wachezaji wake kuangalia 'CD' za baadhi ya michezo yao.
Zahera alisema anatambua umuhimu wa mchezo huo na anaamini wapinzani wake wamejipanga kuwaadhibu kutokana na kuwa na matokeo mabaya katika siku za karibuni.
Alisema anamshukuru Mungu amerudi katika kikosi na kuikuta timu ikiwa katika utimamu mzuri anatarajia kutumia siku moja iliyobaki kuwasoma wapinzani wake.
"Nimerudi jana usiku leo nilikuwa pamoja na timu mazoezini namshukuru msaidizi wangu Noel Mwandila kuyafanyia kazi maagizo niliyomuachia naamini yatakuwa chachu ya muendelezo wa ushindi katika mchezo wetu wa Jumamosi," alisema Zahera.