Yanga waalikwa kuiona Simba ya Uturuki Uwanja wa Taifa

Tuesday August 7 2018

 

Dar es Salaam. Mashabiki wa Yanga wamepewa mwaliko mzito Siku ya kilele cha Maadhimisho  ya Simba Day ambayo yanatarajiwa kufanyika kesho Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kupitia EFM Radio, Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili Simba, Suleiman Kova amewaomba wanachama na mashabiki wa Simba pamoja na Yanga, kujitokeza kwa wingi ili kuweza kushuhudia soka la nguvu kutoka kwa timu yao ambayo ilikuwa Uturuki kwa kambi ya wiki mbili.

Pia mwenyekjiti  huyo anayesimamaia maadili Simba, amewataka Yanga kujipanga upya ili waweze kurejea katika hali yao ya mwanzo.
Amesema ushindani baina ya Simba na Yanga huleta chachu kubwa pale timu hizo mbili zinapokuwa zipo vizuri.
Kova amesema hayo kutokana na mwenendo ambao walionao Yanga kwa kipindi hiki ambapo wanapitia mpito ambao unawafanya hata baadhi ya mashabiki wa timu hiyo kuvunjika moyo.