Yanga ndo imeanza hivyo

Muktasari:

Bao la Mapema lilifungwa na kiungo wa Yanga, Raphael Daud ni kama liliamsha wachezaji wenzake

 TIMU ya Yanga ilikuliona kuliona lango la Mbao FC dakika 16 baada ya kiungo Raphael Daud kuweka mpira wavuni.
Daud aliweka wavuni baada ya Ibrahim Ajib kupiga krosi na Daud kuionganisha kwa kichwa.
Katika mchezo huo Mbao walianza kwa kushambulia langoni mwa Yanga, hata hivyo mabeki wa Yanga walionyesha utulivu.
Goli hilo ni kama liliwaamsha Yanga kwani walianza kucheza kwa madoido na kuonyesha soka safi.
Dakika 22 Mbao walifanya mashambulizi mfululizo ya piga nikupige lakini mabeki wa Yanga waliutoa mpira na kuwa kona isiyokuwa na faida.
LICHA ya kwamba Mbao walikuwa nyuma kwa goli moja dhidi ya Yanga, timu hiyo ya Kanda ya Ziwa walionyesha kutafuta goli la kusawazisha.
Pacha ya Pastory Athanas na Said Jr ilikuwa ikiwahenyesha mabeki wa Yanga na kuwafanya kuwa bize muda wote.
Mbao walikuwa wakitengeneza nafasi nyingi lakini uzoefu ulikuwa ukionekana kuwasumbua katika umaliziaji.
Watoto wa Amri Said walikuwa wamelitawala eneo la katikati na kuwapoteza viungo wa Yanga.

Hata hivyo mchezo huo ulimaliza dakika 90 baada ya Ibrahim Ajib kushindilia msumari wa mwisho na kuifanya Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Katika safu ya kiungo Yanga kulikuwa na mabadiliko baada ya kukosekana Papy Tshishimbi na kuanza Raphael Daud, Feisal Salum na Ajib ambaye alikuwa anatokea juu na kushuka chini.