Yanga huko Zenji haipoi

Muktasari:

Jamhuri ndiyo walikuwa wa kwanza kutikisa nyavu za Yanga kupitia Haji Ramadhan aliyefunga dakika ya 3 tu tangu mchezo kuanza ikiwa ni uzembe wa kipa wa Yanga, Ibrahim Hamid.

Yanga anacheza mechi ya mwisho ya kukamilisha ratiba ya kundi B kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi ambapo kipindi cha kwanza imeshinda mabao 3-1.

Ushindi huo kwa Yanga kama utaendelea hivyo hadi dakika ya mwisho wa mchezo napo hautawasaidia kwani tayari wameondolewa kwenye michuano hiyo.

Jamhuri ndiyo walikuwa wa kwanza kutikisa nyavu za Yanga kupitia Haji Ramadhan aliyefunga dakika ya 3 tu tangu mchezo kuanza ikiwa ni uzembe wa kipa wa Yanga, Ibrahim Hamid.

Faraji Kilaza aliisawazishia Yanga dakika ya 20 akipokea pasi ya Pius Buswita lakini dakika ya 28 Cleofas Kilaza aliongeza bao la pili kwa Yanga.

Yanga waliendelea kutakata kwani dakika ya 32, Buswita alifunga bao la tatu kwa shuti ambalo lilikwenda nyavuni moja kwa moja na kuifanya Yanga kwenda mapumziko ikiongoza mabao 3-1.

Katika kipindi hicho cha kwanza kocha wa Yanga Noel Mwandila alifanya mabadiliko kwa kumtoa Kilaza nafasi yake ilichukuliwa na Cheda Hussein.