Yanga Princess haooooo wanyakua ubingwa, watinga Ligi Kuu

Muktasari:

Yanga Princess imeibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Tanzanite Queens mabao yaliyopatikana dakika ya 26, 32 kwa upande wa Yanga yote yalifungwa na Tabea Aidano na la kufutia machozi kwa upande wa wapinzani wao lilifungwa na Agness Pollangyo.

BAADA ya Yanga Princess kufanikiwa kutwaa kombe la Ligi Daraja la Kwanza sasa wameanza mchakato mzito kuelekea Ligi Kuu ya Wanawake Bara.
Kocha Mkuu wa timu hiyo, Maalim Saleh alisema tayali wameanza mchakato wa kusajili wachezaji kutoka katika timu zilizoonyesha upinzani kwao.
Yanga Princess imeibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Tanzanite Queens mabao yaliyopatikana dakika ya 26, 32 kwa upande wa Yanga yote yalifungwa na Tabea Aidano na la kufutia machozi kwa upande wa wapinzani wao lilifungwa na Agness Pollangyo.
Kocha wa Yanga Princess alisema timu yake ni kubwa inaweza kusajili popote na mchezaji yeyote wanaemtaka.
"Tunampango wa kuwaacha wachezaji kumi na kusajili kumi ambao tunaweza kuwachukua katika timu yoyote ikiwemo Simba,".