Yanga! Hawa ndio wanaumia aisee

Tuesday April 16 2019

 

By Bertha Ismail

ARUSHA.KATIBU Mkuu wa Tawi la Yanga jijini hapa, Bahati Lumato amesema, katika uchaguzi mkuu ujao, wanahitaji viongozi wenye uwezo wa kuikwamua klabu yao kiuchumi kwa sababu timu inapoyumba wanaoumia ni wao mashabiki na wanachama.

Uchaguzi huo umepangwa kufanyika Mei 5 mwaka huu ambapo kampeni zinatarajia kuanza wiki ijayo baada ya hatua zote kukamilika.

Lumato alisema wanasubiri majina ya wagombea yatangazwe ili kuanza kusikiliza sera zao kama kweli wagombea hao wana malengo ya kuitoa Yanga katika hali mbaya ya kiuchumi au kujinufaisha wenyewe.

“Hapa tunasubiri kwanza majina kama wana sifa na kama wanazo tutasikiliza pia sera watakazozinadi wagombea maana hizo zitaweza kutoa mwanga,” alisema Lumato

“Ukata uliopo Yanga hivi sasa umesababishwa na viongozi waliokuwepo, hivyo niwasihiwanachama wenzangu kuwa makini kuwasikiliza kama wana mapenzi mema na klabu yetu.”

Lumato aliongeza mwaka huu wanafanya uhamasishaji mkubwa kwa mashabiki na wapenzi wa Yanga kujisajili na kuwa wanachama ili wapate sifa za kupiga kura uchaguzi huo.

Advertisement