Yaani Omog yupo tu Cameroon!

Muktasari:

  • Kocha mkuu wa zamani wa Simba, Mcameroon Joseph Omog amesema, yupo tu nyumbani kwao na hajapata timu ya kufundisha yenye maslahi mazuri.

Dar es Salaam. Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog kwa sasa yupo ametulia tu nyumbani kwao Younde, Cameroon kwa sababu hajapata timu ya kufundisha yenye maslahi mazuri.

Omog kocha aliyezinoa klabu za Tanzania za Azam FC ambayo aliipa ubingwa msimu wa 2013- 2014 na Simba aliyoicha kwenye nafasi nzuri ya kuchukua ubingwa na baadaye waliutwaa katika kipindi cha msimu uliopita.

"Kwa sasa nipo tu nyumbani sijapata timu ya kufundisha. Ni kwa sababu ofa zilizokuja mezani kwangu sikupenda nikaamua nipumzike nicheze na wajukuu,"alisema Omog.

Amesema, kama kuna timu nyingine nzuri ambayo ina maslahi safi anaweza kufundisha.

Kocha huyo, aliondolewa Simba katika mazingira ya kutatanisha hasa baada yaiongoza klabu hiyo vizuri bila kupoteza mechi hata moja.