Breaking News
 

Wenger aja na mpya kuhusu Giroud

Monday December 11 2017

 

London, England. KOCHA wa Arsene Wenger, amesisitiza kwamba nyota wake Olivier Giroud hauzwi na kuwa klabu ambazo zimekuwa zikimnyemelea kwa lengo la kumsajili mwezi Januari zisahau suala hilo.

Mchezaji  huyo amekosa nafasi za kucheza mara kwa mara msimu huu lakini wikiendi alitoka benchi na kufunga bao la kusawazisha wakati kikosi chake kilipotoka sare ya 1-1 na Southampton.

Hilo lilikuwa bao lake la nne katika mechi 13 alizocheza akiingia kutoka benchi. Suala la kukosa nafasi ya mara kwa mara limemfanya nyota huyo akifikirie kutaka kuondoka. Na wakati akifikiria suala hilo, Wenger kwa upande wake hataki nyota huyo aende.

“Ni kwa nini tupoteze mchezaji muhimu?” aliuliza kocha huyo wakati akimzungumzia Giroud ambaye alikuwa akikaribia kujiunga na Everton mwishoni mwa msimu uliopita.

“Ataanza kucheza katika kikosi cha kwanza. Unajua unapokuwa  na wachezaji wengi wazuri kuna wengine hawataanza kwenye kikosi cha kwanza.

“Na kila mara utaulizwa; Hivi mbona mchezaji fulani ni mzuri lakini hachezi?”