Wema na Aunt Ezekiel wanapobadilika kama kinyonga

Tuesday August 13 2019

 

By Rhobi Chacha

Hakuna asiyefahamu kuwa waigizaji wa filamu Aunt Ezekiel na Wema Sepetu kuwa sio marafiki.

Lakini miaka mitatu iliyopita wawili hao walikwaruzana na kila mmoja alitangaza kuwa hawahitaji marafiki tena katika maisha yao.

Ikaja konekana tena wawili hao wako pamoja na kudai ile ilikuwa ni utoto hivyo wamekaa chini na kuanza upya urafiki wao.

Chakushangaza Julai 4,2019  Wema Sepetu alipofutiwa shtaka la kusambaza video isiyo na maadili na kuachiwa huru alitangaa hataki marafiki kwa kuwa hawamsaidii chochote hivyo kwa sasa rafiki yake mkubwa ni familia yake.

Kauli hiyo iliwastua watu na kuanza kujiuliza kulikoni  urafiki wao na Aunt Ezekiel? Hapa MCL Digital lilimtafuta Aunt na kumuuliza swali hilo ambapo alijibu hivi:

“Aise kwanza mimi binafsi sijaisikia hiyo kauli aliyoiongea Wema,na sijui kama kamaanisha ni rafiki yupi sababu mimi na Wema sio marafiki bali tumekuwa kama ndugu,yaani tumeshatoka kwenye urafiki kitambo kwa kweli

Advertisement

“Na hiyo ya kusema tunabarika kwa kutamka kauli hii ya kutotaka marafiki,hii hutokeaga tu pale unapoona unamchukulia mtu kama rafiki lakini kumbe sio mtu mzuri kwako,hivyo hata kama Wema alisema hivyo yuko sahihi mimi namsapoti sana”alisema Aunt

Aisha Aunt aliendelea kusema hata yeye hataki marafiki kwani haoni faida yao,hivyo akionekana yupo karibu na mtu watu wajue huyo sio rafiki ni ndugu.

Advertisement